Maaskofu wa katoliki nchini wametoa wito kwa kinara wa Azimio Raila Odinga kusitisha maandamano

  • | K24 Video
    215 views

    Maaskofu wa katoliki nchini wametoa wito kwa kinara wa Azimio Raila Odinga kusitisha maandamano ya kila jumatatu na alhamisi wakisema maandamano hayo yamepekelea uharibifu wa mali, na kuhatarisha maisha ya wananchi. Aidha, pia wanataka upande wa serikali usitishe mikutano ya maombi, wakidai inapandisha joto la kisiasa nchini. wamezungumza kupitia mwenyekiti wake martin kivuva ambaye ni askofu mkuu wa Mombasa, semi zake zikiungwa mkono na maaskofu wa Nyeri, Kirinyaga, Eldoret, na maeneo mengine nchini.