Mabwawa ya Seven Forks, yameendelea kujaa kwa kasi

  • | Citizen TV
    6,077 views

    Siku mbili baada ya serikali kutoa tahadhari ya mafuriko kwa wakaazi wanaopakana na mabwawa yaliyo kwenye hatari ya kuvunja kingo, bwawa la Masinga sasa limejaa pomoni. Kulingana na taarifa iliyochapishwa hii leo, bwawa hilo limenakili viwango vya juu zaidi katika historia kufuatia ongezeko la mvua humu nchini. Haya yanajiri huku naibu rais Rigathi Gachagua akibaini kuwa serikali itatoa takriban shilingi bilioni 1.2 kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko