- 5,828 viewsDuration: 3:45Machifu Watano waliotekwa nyara na kundi la kigaidi Al Shabaab na kusafirishwa nchi jirani Somalia kwa jumla ya miezi miwili wamesimulia masaibu yao mikononi mwa magaidi hao. Machifu hao waliokuwa mateka kwa zaidi ya miezi miwili wanaitaka serikali kuwasadia kwani familia zao zinateseka. Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amehakikishia Machifu hao na wengine walioko kwenye mpaka wa Kenya na Somalia kwamba mahitaji yao yatashughulikiwa.