Madaktari wanagenzi wasitisha kambi nje ya wizara ya afya

  • | KBC Video
    2 views

    Madaktari wanagenzi wanaogoma wamesitisha hatua yao ya kukita kambi kwenye wizara ya afya ili kufanikisha mashauriano baina ya wizara hiyo na chama cha madaktari na wataalamu wa meno na dawa nchini kinachotetea haki zao. Wanagenzi hao ambao wamekuwa wakikita kambi kwneye makao makuu ya wizara hiyo wanataka utekelezaji wa mkataba wa makubaliano ya pamoja wa mwaka 2017 wakisema wataendelea na maandamano yao Jumatatu ijayo iwapo malalamishi yao hayatashughulikiwa. Haya yanajiri huku waziri wa afya Susan Nakhumicha akidai kwamba kundi la watu fulani linapanga njama ya kuiharibia wizara hiyo sifa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive