- 18,298 viewsDuration: 3:27Maelfu ya watu wamesalia bila makao katika sehemu mbali mbali nchini, huku mali ya thamani isiyojulikana ikiharibiwa na mafuriko. Katika kaunti ya Kismu, zaidi ya nyumba mia tatu zilisombwa na maji, baada ya mito Nyando na Awach kuvunja kingo. Vile vile, mamia ya wasafiri walitatizikia katika kaunti za Kericho, Makueni, Migori na Narok, huku Mamlaka ya kitaifa ya barabara KeNHA ikitoa tahadhari katika sehemu mbali mbali.