Maelfu ya wapalestina wamejihifadhi katika hospitali ya Al-Shifa

  • | VOA Swahili
    46 views
    kituo kikubwa cha matibabu huko Ukanda wa Gaza ambacho hivi karibuni kilikumbwa na amri ya Israel kutaka watu waondoke. Lakini raia, wakiwa kwenye mahema katika eneo la hospitali, wanasema hawana pa kwenda, na hawapangi kuondoka. Vibanda vya vyakula na nguo vimewekwa kuzunguka hospitali. Mwanamke mmoja asiyekuwa na makazo, Om Haitham Hejela, anasema hali ni mbaya sana hapo hospitali lakini anasisitiza kwamba hataondoka hospitali ya Al-Shifa kwa vile hana kwingine kwa kwenda. Jeshi la Israel limelishutumu kundi la harakati za Kiislamu Hamas siku ya Ijumaa (Oktoba 27) kwa kuitumia hospitali kuu huko Gaza kama ngao kwa ajili ya mahandaki na vituo vyao vya operesheni. Afisa wa Hamas Ezzat El-Reshiq, mwanachama wa kitengo cha harakati za kisiasa, alisema kwenye Telegram: “Hakuna ukweli kwa kile ambacho kimeripotiwa na msemaji wa jeshi la adui,” akiishutumu Israel kwa kusambaza uongo kama “utangulizi wa kutenda maafa makubwa mapya dhidi ya watu wetu.” Hospitali hivi sasa ni makazi ya wapalestina takriban 50,000 wasiokuwa na makazi, maafisa wa afya wanasema. Maafsia wa afya katika hospitali za Al-Shifa na Al-Quds wamesema mashambulizi ya anga yamepiga karibu na majengo yao. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu OCHR imesema raia 117,000 wanahifadhiwa pamoja na maelfu ya wagonjwa na madaktari katika hospitali za kaskazini. #Alshifa #israel #voa #reels #igreels #videography #hezbollah #hamas #gaza #shambulizi #hamas #benjaminnetanyahu #wazirimkuu