Maeneo maalum kufunguliwa katika maeneo kame kushughlikia lishe ya mifugo

  • | KBC Video
    9 views

    Zaidi ya wafugaji elfu-moja kutoka maeneo kame humu nchini wanatarajiwa kunufaika na mradi utakaoshughulikia athari za ukame katika maeneo hayo. Mradi huo utashirikisha ufugaji na kilimo kwa lengo la kufanikisha kutengwa kwa maeneo ya malisho katika wadi 490 katika maeneo kame ambapo ukame umesababisha maafa makubwa kwa watu na mifugo.Akiongea katika kaunti ya Marsabit wakati wa kikao cha kukusanya maoni ya umma kuhusu mradi huo ,katibu katika wizara ya ustawi wa maeneo kame Harsama Kello alisema kuwa mradi huo utagharimu shilingi milioni 13 ambazo zitagharamia juhudi za kuimarisha mifugo na kujenga vyanzo vya maji miongoni mwa miradi mingine ya manufaa kwa jamii. Katika kaunti ya Marsabit mradi huo uliogharimu shilingi bilioni 2.7 uko katika ardhi ya ekari elfu-12 na unatarajiwa kushughulikia mifugo elfu-2 . Kaunti nyingine zitakazopewa kipaumbele ni Garissa, Mandera, Tana River, Isiolo, Samburu, Turkana, Baringo, West Pokot na Wajir.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive