Mafuriko Somalia yawaacha watu 300,000 bila makazi

  • | VOA Swahili
    159 views
    Umoja wa Mataifa umeyaelezea mafuriko yamewabandua maelfu ya watu makwao nchini Somalia pamoja na mataifa mengine ya AFrika Mashariki kufutia kipindi cha ukame cha kihistoria kilichotokea mara moja karne. Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, takriban watu milioni 1.6 nchini Somalia huenda wakaathiriwa na mvua kubwa za msimu ambazo pia zimechochewa na matukio mawili ya kutokana ya mabadiliko ya hali ya hewa, mvua za El Nino na Dipole kwenye bahari Hindi, kulingana taarifa ya Alhamisi kutoka ofisi ya UN inayoratibu masuala ya kibinadamu, OCHA. Mafuriko hayo yaliyofuatiwa na mvua kubwa zilizoanza mapema mwezi uliopita tayari yameua takriban watu 29 na kuwalazimisha wengine zaidi ya laki 3 kuhama makwao nchini Somalia, huku miji na vijiji vikisombwa na maji.