Skip to main content
Skip to main content

Magavana wa pwani wafoka wakitaka kuvunjwa kwa mamlaka ya maji

  • | Citizen TV
    220 views
    Magvana wanne kutoka kaunti za Pwani wanaotegemea maji kutoka kwa Mamlaka ya usambazaji maji Pwani sasa wanataka kuvunjiliwa mbali kwa bodi ya mamlaka hiyo kwa madai ya utepetevu. Magavana hao Gideon Mung’aro wa Kilifi, Abdulswammad Nassir wa Mombasa, Andrew Mwadime wa Taita Taveta na naibu gavana wa Kwale Chirema Kombo wanasema mamlaka hiyo imezembea katika utendakazi wake huku wananchi wakiendelea kutaabika kwa kukosa maji kutokana na kutorekebishwa kwa mabomba ya usambazaji maji katika maeneo mbali mbali. Kulingana na magavana hao, hali kwa sasa katika kaunti hizo ni mbaya zaidi kutokana na kiangazi kinachoshudiwa nchini akisema licha ya kufanya mazungumzo na Wizara ya maji Pamoja na maafisa wakuu wa mamlaka hiyo, hakuna mabadiliko yoyote yaliyoshuhudiwa.