Magavana walalamikia uhaba wa fedha kwenye kaunti

  • | Citizen TV
    634 views

    Baadhi ya kaunti nchini sasa zimelazimika kuchukua mikopo kutoka kwa benki kulipa mishahara ya wafanyakazi wao, baada ya kukosa fedha za kuendesha shughuli zao. Wakizungumza baada ya mkutano wa magavana na Naibu Rais Rigathi Gachagua hapa Nairobi, magavana hao sasa wanasema, huenda hali ikawa mbaya hata zaidi baada ya mswada wa fedha wa mwaka wa 2024 kuangushwa.