Skip to main content
Skip to main content

Mahakama imeamuru kesi inayohusu mali ya marehemu Jaji David Majanja isikizwe

  • | Citizen TV
    600 views
    Duration: 59s
    Mahakama imeamuru kesi inayohusu mali ya marehemu Jaji David Majanja isikizwe haraka kufuatia kudhoofika kwa afya ya mmoja wa walalmishi katika kesi hiyo, Gerishon Majanja... Kesi hiyo ilikuwa imesikizwa na Jaji Chemitei ambaye aliamuru pande zote kuwasilisha stakabadhi zaidi ili kutoa maelezo zaidi kuhusu baadhi ya maswala ya kesi hiyo. Mawakili wa pande zote waliiomba mahakama kuharakisha kesi hiyo kutokana na hali ya kiafya ya mmoja wa walalamishi. Mahakama ikiarifiwa kuwa hali ya Mzee Gerishon ambaye ni babake Jaji Majanja inaendelea kudhoofika na kwamba kesi hiyo isikizwe bila kuahirishwa zaidi. Mahakama ilikubali ombi hili na kuamuru kesi iwasilishwe mara moja mbele ya Jaji msimamizi kwa mwelekeo zaidi..