Skip to main content
Skip to main content

Mahakama ya Rufaa yatangua uamuzi wa mahakama Kuu kuhusu hazina ya NG-CDF

  • | Citizen TV
    68 views
    Mahakama ya Rufaa imebatilisha uamuzi wa Mahakama Kuu uliokuwa umetangaza Sheria ya hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge, maarufu kama NGCDF, kuwa kinyume na Katiba, na kuamuru kusitishwa kwa mfuko huo. Katika uamuzi muhimu uliotolewa leo, Mahakama ya Rufaa iliweka kando uamuzi ya Mahakama Kuu ya tarehe 20 Septemba 2024, na ikaamua kuwa Sheria ya NGCDF ya mwaka 2015 bado ni halali kikatiba kwa sehemu kubwa. Majaji wa Mahakama ya Rufaa walisema Mahakama Kuu ilikosea kwa kubatilisha sheria nzima, wakionya kuwa hatua hiyo ilikuwa kali kupita kiasi na ingeathiri vibaya miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na hazina hiyo kote nchini.