Mahakama yaharamisha shule kutoza ada za ziada

  • | Citizen TV
    229 views

    Mahakama Kuu imeamua kuwa ni haramu kwa shule za umma nchini kuwatoza wanafunzi ada za ziada bila idhini ya waziri wa elimu. Uamuzi huu ukifuatilia kesi iliyowasilishwa dhidi ya shule ya upili ya wasichana ya St. Georges kwa madai ya kuwataka wazazi kulipa ada zaIDI. Kwenye uamuzi wake, mahakama imeamua kuwa hakuna shule ya umma inayoruhusishwa kuongeza karo au kulipisha ada kinyume na sheria ya elimu ya msingi na sekondari. Kwenye kesi hii, mahakama ilibaini kuwa shule ya St Georges ilikuwa imewataka wazazi kulipa pesa kadhaa ikiwemo mradi wa ujenzi wa bweni, miundo msingi na hata kufidia uchache wa bajeti ya shule