Mahakama yasitisha mpango wa serikali wa kusajili watu na kutoa vitambulisho vipya vya kidijitali

  • | K24 Video
    22 views

    Mahakama kuu imesitisha mpango wa serikali wa kusajili watu na kutoa vitambulisho vipya vya kidijitali kusubiri matokeo ya kesi ya taasisi ya katiba isikizwe na kuamualiwa. Mahakama katika uamuzi wake imekubaliana na hoja ya taasisi ya katiba kwamba serikali haina msingi wa kisheria wa kutekeleza utoaji wa maisha namba, na kwamba imeendelea bila kuhitaji tathmini ya athari ya ulinzi wa data, kinyume na sheria.