Skip to main content
Skip to main content

Mahujaji wa Kiislamu waelekea Mlima Arafat kuadhimisha siku kuu ya Hija

  • | Citizen TV
    85 views
    Mahujaji wa Kiislamu walioko nchini Saudi Arabia wameondoka alfajiri ya leo kuelekea katika Milima ya Arafat kuadhimisha siku inayochukuliwa kuwa muhimu zaidi katika ibada ya Hija. Waumini hao wameonekana wakitembea kuelekea eneo la Jabal Arafat huku wengine wakipanda milimani wakati wa alfajiri, katika eneo ambalo inaaminika Mtume Muhammad alitoa hotuba yake ya mwisho zaidi ya miaka zaidi ya elfu moja na mia nne iliyopita. Ibada ya Hija, ambayo ni wajibu kwa kila Muislamu mwenye uwezo, inakisiwa kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi wa kidini duniani. Mwaka huu zaidi ya mahujaji milioni tatu wamekusanyika nchini Saudi Arabia kwa ibada hiyo. Mahujaji watasalia Arafat hadi machweo kabla ya kuelekea Muzdalifah, ambako watakusanya vijiwe kwa ajili ya ibada ya kupiga mawe nguzo zinazowakilisha shetani. Ibada hiyo inaashiria mwanzo wa sikukuu ya Eid al-Adha, ambayo itaadhimishwa na Waislamu kote duniani kesho.