Makadinali 133 wakongamana Vatican kumchagua papa

  • | Citizen TV
    594 views

    Makadinali 133 wamekongamana katika kanisa la Sistine, mjini Vatican kwa matayarisho ya kura ya kumchagua Papa mpya atakayeongoza kanisa Katoliki duniani. Shughuli ya kumchagua mrithi wa Papa marehemu Francis inaanza leo. Tayari makadinali watakaoshiriki uchaguzi wamekula kiapo. Moshi mweupe utakapofuka kwenye dohani ya kanisa la St Peter's utaashiria kupatikana kwa papa mpya.