- 4,209 viewsDuration: 2:52Huzuni na majonzi zilishamiri kwenye makafani ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga, familia za watu 22 walipokezwa miili ya wapendwa wao ili kuisafirisha kwa mazishi. Watu hao ni kati ya 27 waliofariki kufuatia ajali katika barabara ya Kisumu kuelekea Kakamega. Familia za marehemu zimeitaka serikali kuimarisha usalama wa barabarani.