Mama na mawanawe wateketea hadi kufa Kiambu

  • | Citizen TV
    1,497 views

    Wingu la simanzi limetanda katika Kijiji Cha Magina eneo bunge la Lari Kaunti ya Kiambu,baada ya mama na mwanawe wa kidato Cha kwanza kuteketea na moto hadi kufa,usiku wa kuamkia leo. Marehemu Esther Njeri aliyekuwa na umri wa miaka 54,alikuwa mama ya watoto watano.Akithibitishwa kisa hicho, naibu chifu wa kata ndogo ya Magina Isaac Muchiri, Kariuki amesema kwamba tayari maafisa wa usalama wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo.kwani majirani waliofika katika nyumba hiyo kujaribu kuwaokoa wanasema mlango wa nyumba ya marehemu ulikuwa umefungwa kwa nje.Tayari mabaki ya wawili hao yamepelekwa katika makafani ya hospitali ya Naivasha kaunti jirani ya Nakuru, kusubiri upasuaji wa maiti kwa uchunguzi zaidi.