Mamia ya wakazi wa kaunti ya mombasa waandamana kushinikiza kusitishwa kwa vita vya Israel na Gaza

  • | K24 Video
    157 views

    Mamia ya wakazi wa kaunti ya mombasa na mashirika ya kijamii wameandamana kushinikiza kusitishwa kwa vita vya Israel na Gaza. Maandamano hayo yamefanyika wakati ambapo israel imeongeza mashambulizi yake Gaza huku idadi ya waliouawa ikiwa zaidi ya 4,500. wakati hayo yakijiri Israel imewataka raia wake walioko Jordan na Misri waondoke mara moja. Hayo yakijiri kongamano la amani la Cairo limeandaliwa leo kujadili jinsi kutuliza vita huku hofu ya mzozo huo kuenea mashariki ya kati ikiongezeka.