Maombi maalumu ya kuombea ukame

  • | BBC Swahili
    184 views
    Kufuatia kuelezwa kwamba janga la ukame huenda likaendelea kuwa baya zaidi katika nchi za pembe ya Afrika na Kenya ambako baa hilo limedumu kwa miaka mingi mfululizo mpaka sasa, hatimaye baadhi ya viongozi wa dini wameibuka na kufanya maombi maalumu. Askofu Charles Gadi wa kanisa la Good news for all ambaye amekuwa akizunguka maeneo mbalimbali dunia kwenda kuomba kwaajili ya majanga kwa sasa amefanya maombi maalumu dhidi ya ukame huo unaokabili maeneo ya Kenya. Akizungumza na Mwandishi wa BBC Leonard Mubali anaelezea namna ambavyo kipaumbele chake ni kuombea majanga #bbcswahili #maombi #ukame