Skip to main content
Skip to main content

Marekani imepiga kura ya turufu katika mswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

  • | BBC Swahili
    10,475 views
    Duration: 50s
    Marekani imepiga kura ya turufu katika mswada wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lingetaka usitishaji vita mara moja huko Gaza. Mswada huo pia ulitaka kuachiliwa kwa mateka wote na kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu kuwafikia Wapalestina waishio Gaza. Hii ni mara ya sita kwa Marekani kupiga kura ya turufu katika kikao hicho kuhusu vita vya takriban miaka miwili kati ya Israel na Hamas. Je, Marekani imetoa sababu gani za kuchukua uamuzi huu na hii iamaanisha nini kwa mzozo unaoendelea? Tunazungumzia hili mwendo wa saa tatu kamili katika Dira ya Dunia ukiwa nami @elizabethkazibure Pia unaweza kufuatilia matangazo haya mubashara katika mitandao yetu ya youtube na facebook ya bbcswahili. - - #bbcswahili #diratv #gaza #marekani