Maseneta na wabunge waitaka serikali kuruhusu kituo cha kibiashara cha China Square kifunguliwe

  • | K24 Video
    134 views

    Baadhi ya maseneta na wabunge wanaitaka serikali kuruhusu kituo cha kibiashara cha China Square kinachokumbwa na utata kifunguliwe. Viongozi hao wamekariri haja ya kulinda wawekezaji wa kigeni ambapo wameshauri serikali kuhakikisha usawa wanaposhughulikia mzozo huo. Wafanyibiashara wa humu nchini pia wametakiwa watumie njia zifaazo katika kutatua mzozo huo.