- 263 viewsDuration: 1:59wakazi wa Busia wamehimizwa kujitokeza kwa wingi na kutoa damu ili kuokoa maisha, kaunti hiyo ikikumbwa na uhaba mkubwa wa damu na kusababisha wagonjwa kusafirishwa hadi katika kaunti jirani za Bungoma, Kakamega na Kisumu kutafuta huduma hizo Hata hivyo, imebainika kwamba baadhi ya wakazi wa Busia hutaka kulipwa kabla ya kutoa damu. Haya yanajiri huku mashabiki wa timu ya Arsenal kaunti ya Busia wakijitokeza kwa wingi mjini Busia na kushiriki katika zoezi la utoaji wa damu .