Mashabiki ashiki kutoka maneo mbalimbali humu nchini walipata fursa ya kuzuru studio za redio za Shirika la Utangazaji nchini, KBC ikiwa ni sehemu ya msururu wa shughuli zilizoandaliwa kuadhimisha wiki ya redio. Wakati wa ziara hiyo, mashabiki walishuhudia utayarishaji wa vipindi na kutangamana na watangazaji wa redio wawapendao wakiwemo manguli na wabobezi waliotia fora katika tasnia ya utangazaji. Pia walijifunza mengi kuhusu mabadiliko ya kimitambo kadri miaka inavyosonga.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive