Mashtaka ya ugaidi dhidi ya Boniface Mwangi yafutwa Kenya

  • | BBC Swahili
    733 views
    Idara ya Upelelezi wa makosa ya Jinai nchini Kenya imetupilia mbali mashtaka yanayohusiana ya ugaidi dhidi ya mwanaharakati Boniface Mwangi. Mwangi sasa anakabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha bila kibali na kupatikana na sumu pamoja na vitoa machozi. Kukamatwa kwake kumekosolewa, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakikosoa kuwa ni kwa lengo la kukandamiza sauti za upinzani. Tuhuma dhidi yake zinahusiana na maandamano ya Juni 25. Wiki iliyopita watu 36 walifikishwa mahakamani kwa shtaka hilo la ugaidi baada ya kushiriki maandamano hayo. Je shtaka la kigaidi linamaanisha nini hasa na ni mtu aina gani anaweza kushtakiwa kwa hili? Jiunge na @Hamida Abubakar saa tatu usiku kwenye Dira ya Dunia TV mubashara kwenye ukurasa wa YouTube BBC Swahili. #bbcswahili #kenya #diratv Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw