Skip to main content
Skip to main content

Mashtaka ya uhaini: Machar, Lissu, Besigye, Kabila kunani?

  • | BBC Swahili
    11,199 views
    Duration: 1:04
    Upinzani wa Sudan Kusini umepuuzilia mbali mashtaka ya uhaini na mauaji dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dk. Riek Machar ukiyataja kama “fitina za kisiasa” zinazotishia makubaliano dhaifu ya amani ya nchi hiyo. Wizara ya Sheria ya Sudan Kusini imetetea uamuzi wake, na kusisitiza kuwa wale waliohusika na ukatili “watawajibishwa, bila kujali nafasi zao au ushawishi wao wa kisiasa.” Sasa kwa nini kesi za aina hii zimekuwa nyingi katika Ukanda wa Afrika Mashariki? Tunaangazia hili mwendo wa saa tatu kamili katika Dira ya Dunia ukiwa nami @elizabethkazibure . Pia unaweza kufuatilia matangazo haya mubashara katika mitandao yetu ya youtube na facebook ya bbcswahili. - - #bbcswahili #sudan #siasaSubscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw