Skip to main content
Skip to main content

Masikonde awashtumu polisi kwa kumdhulumu

  • | Citizen TV
    587 views
    Duration: 2:06
    Bunge la Kaunti ya Narok liligeuzwa kuwa uwanja wa mabishano wakati mwakilishi wadi wa Narok Town Douglas Masikonde alipokuwa akitoa hotuba yake ya shukrani kwa kuchaguliwa kuwakilisha wakazi katika bunge hilo. Masikonde alionekana kuwazomea maafisa wa usalama waliomvamia nyumbani kwake usiku wa kuamkia siku ya upigaji kura na wakiwapiga maajenti wake.