- 101 viewsDuration: 2:01Changamoto za ukosefu wa ajira, Miundo mbinu duni ya elimu ni miongoni mwa sababu zilizotajwa kuchangia viwango vya elimu eneo bunge la Lamu Mashariki kuendelea kudorora. Katika mtihani wa kitaifa KCSE wa mwaka jana kati ya wanafunzi 250 waliofanya mtihani huo kwenye shule sita za upili zilizoko eneo hilo,wanafunzi 93 walipata alama ya E. Wakizungumza Kisiwani Amu wadau wa elimu wa Lamu Mashariki wametaka viongozi wa Lamu kushirikiana ili kuboresha elimu katika eneo bunge hilo.