- 6,254 viewsDuration: 1:19Mawakili wa mshukiwa wa mauaji ya Tob Cohen, Sarah Wairimu, wamezua maswali kuhusu kuhusishwa kwa vijana wasio maafisa wa polisi katika kuondoa mwili wa Cohen kutoka kwenye tenki la maji la ardhini katika boma lake, mtaa wa Kitisuru. Wakili wa Wairimu, Christine Kariuki, akimhoji shahidi aliyerekodi video wakati mwili huo ulipopatikana, alitaka kufahamu kwa nini polisi waliruhusu raia kuwa karibu na eneo la tukio na kushiriki katika shughuli hiyo. Kwa upande wake, mtaalamu wa uchunguzi wa video, Beneutychus Wanjohi, alisema hakuhitilafiana na uchunguzi huo kwani walifanya kazi chini ya mwongozo wa maafisa wa upelelezi. Afisa huyo pia alieleza mahakama kuwa kwa siku mbili alinasa maafisa wenzake wakitafuta ushahidi kabla ya mwili wa Tob Cohen kupatikana tarehe 13 Septemba, 2019.