Mawaziri wateule waendelea kupingwa

  • | K24 Video
    444 views

    Wakati tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maoni ya umma kuhusu uteuzi wa mawaziri wa baraza la mawaziri inakaribia, kuna ongezeko la shughuli kutoka kwa makundi ya kiraia na watu binafsi. aliyekuwa mwakilishi mkuu wa kinara wa Azimio Raila odinga wakati wa uchaguzi, Saitabao Ole Kanchory, amejiunga na orodha ya wale wanaopinga uteuzi huo mahakamani, anadai kwamba uteuzi wa viongozi wa upinzani katika baraza la mawaziri unadhoofisha jukumu lao la kikatiba la kusimamia na kukosoa serikali. Aidha, harakati za kiraia zinazoongozwa na mawakili zinahamasisha vijana kuunga mkono ombi la kupinga uteuzi huo.