Mazishi ya Padre Cheruiyot

  • | Citizen TV
    3,088 views

    Familia, jamaa na viongozi wanataka kukamatwa kwa wahusika wa mauaji ya padre Allois Cheruiyot wa kanisa katoliki aliyeuawa na majangili tarehe 22 mwezi uliopita. Katika hafla ya mazishi iliyofanyika katika uwanja wa shule ya wavulana ya ST Michael Terige waliozungumza waliungana kwa semi moja kukashifu mauaji ya padre huyo ambaye licha ya kuwa mwanga wa amani na umoja eneo la Kerio Valley maisha yake yalikatizwa ghafla.