Mbio za Chepsaita zazinduliwa Uasin Gishu

  • | Citizen TV
    530 views

    Mbio za nyika za Chepsaita zitakazoandaliwa kwa mara ya kwanza mwezi Disemba katika kaunti ya Uasin Gishu zimezinduliwa rasmi hii leo. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, msimamizi Farouk Kibet amesema mipango yote imekamilika akiwataka washiriki kujiandaa kwa shindano kali zaidi katika eneo hilo la Chepsaita. Kibet alikuwa ameandamana na waziri wa michezo Ababu Namwamba, katibu wake Peter Tum na gavana wa Uasin Gishu Jonathan Bii. Mshindi wa dunia wa medali ya fedha Margaret Chelimo ni miongoni mwa wanariadha tajika watakaoshiriki.