Mbio za kupanda daraja ya FKF

  • | Citizen TV
    104 views

    Mbio za kupandishwa daraja hadi ligi kuu ya FKF zimeongeza kasi huku timu nne zikiwa katika kinyang'anyiro cha kuchukua nafasi mbili zilizosalia. Fortune sacco iliongeza matumaini yao ya kupandishwa daraja kwa kuwafunga 3k fc 2-1 jana alasiri na kudhibiti nafasi ya tatu. Vijana wa migori youth wameongeza matumaini ya kusalia nsl baada ya ushindi mgumu wa 1-0 dhidi ya luanda villa kwenye uwanja wa migori. Migori walifunga bao la pekee kupitia penalti ya kipindi cha kwanza. Migori ilipaswa kushinda kwa mabao mengi, lakini hawakuweza kutumia nafasi zao. Huku vijana wa ss assad na muhoroni wakiwa tayari wameshuka daraja, timu tatu, migori youth, mombasa elite na mombasa stars wanapigania kubaki daraja la pili.