Mbunge Farah Maalim kufika mbele ya tume ya NCIC

  • | KBC Video
    37 views

    Tume ya uwiano na mshikamano wa taifa imetaka mbunge wa Dadaab Farah Maalim kufika mbele yake kuangazia matamshi tata anayodaiwa kutoa kuhusu maandamano ya hivi majuzi. Mbunge huyo ameagizwa ajiwasilishe katika afisi tume hiyo kesho saa tano asubuhi, na asipofanywa hivyo atakamatwa. Katika video iliyosambaa mtandaoni, mbunge huyo alisikika akidaiwa kusema kuwa kama angekuwa Rais angekabiliana na waandamanaji bila huruma. Na kama vile mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim anatuarifu, baraza la kitaifa la chama cha Wiper limeafikiana kumuondoa Maalim katika kamati zote za bunge kufuatia matamshi hayo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive