- 6,982 viewsDuration: 1:46Mbunge wa Kitutu Chache Kusini Anthony Kibagendi amejipata taabani kufuatia matamshi yake alipodai kuwa bunge limenadiwa kwa serikali. Kibagendi kwenye kipindi cha daybreak hapa citizen alimshutumu spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula na manaibu wake alidai wanaharibu na kulivuruga bunge la kitaifa. Spika Wetangula aliyekerwa na matamshi hayo alimfurusha Kibagendi bungeni na kuamuru asiruhusiwe kwenye vikao vya bunge na vya kamati hadi pale atakapoomba msamaha rasmi