Mbunge Peter Salasya asema masaibu yake yamechochewa kisiasa

  • | KBC Video
    351 views

    Ikiwa ni siku moja pekee baada ya Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini(EACC) kumtaka Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya kufika mbele yake ili kuchunguzwa kuhusiana na madai ya kumshambulia mwakilishi wadi wa Malaha-Isongo Peter Walunya, mbunge huyo sasa anadai hatua ya EACC imechochewa kisiasa. Akiongea katika hafla moja ya maombolezo huko Eluche eneo bunge lake, Salasya amesema anashangaa ni vipi tume ya EACC inafuatilia suala hilo ilhali kesi hiyo bado inashughulikiwa mahakamani, akidai hatua hiyo inachochewa na mahasimu wake wa kisiasa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive