Mbunge wa Uturuki avunja simu yake kwa nyundo bungeni

  • | BBC Swahili
    1,506 views
    Mbunge wa Uturuki amevunja simu yake ya mkononi kwa nyundo alipokuwa akizungumza bungeni. Burak Erbay, ambaye ni mwanachama wa chama cha upinzani cha Republican People's Party, alikuwa akipinga mswada unaoungwa mkono na serikali ambao unanuia kupambana na "taarifa potofu". Chini ya sheria hiyo, mitandao ya kijamii na tovuti zitalazimika kutoa maelezo ya watumiaji wanaoshukiwa "kueneza habari za kupotosha". #bbcswahili #uturuki #uhuruwahabari