Meli iliyobeba abiria 800 kutoka nje yawasili bandarini Mombasa

  • | K24 Video
    154 views

    Bandari ya Mombasa imepokea meli ya abiria iliyowabeba wageni zaidi ya 800 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni. Meli hiyo kwa jina Mv Bolette ilitia nanga mwendo wa saa nane usiku. Watalii wanatarajiwa kuzuru maeneo tofauti ya kitalii huko pwani pamoja na kuelimishwa kuhusu utamaduni wa wakazi.