Mfanyakazi mlemavu alala afisini kupinga kuhamishwa katika jumba la Harambee

  • | Citizen TV
    3,498 views

    Mfanyikazi mmoja wa serikali amelala ndani ya afisi yake katika jumba la Harambee ambayo pia ni ofisi ya Rais ili kuzuia afisi yake kuvunjwa kwa ukarabati. Phyllis Anyango Ouko ambaye anafanya kazi katika afisi ya katibu wa usimamizi katika wizara ya usalama wa kitaifa ametakiwa kuhama kutoka ghorofa ya kwanza hadi ya nane. Lakini Phyllis ambaye ni mlemavu na anatumia gari la magurudumu anasema ataathirika iwapo kambarau zitaharibika wakati wa dharura akisema juhudi za kumuomba mkuu wa utumishi wa Umma Felix Kosgei kumsikiza zimeambulia patupu