Mgomo wa madaktari kufika siku 22

  • | Citizen TV
    212 views

    Katibu wa wizara ya afya Mary Muriuki amewataka madaktari kurejea kwenye meza ya mazungumzo bila vikwazo ili kukwamua mazungumzo ambayo yamesambaratishwa na pande zote mbili kuchukua misimamo sugu. akizungumza kwenye warsha ya siku tatu ya maafisa wa afya nyanjani, Muriuki amesema kuwa serikali imejaribu kutimiza baadhi ya malubaliano kwenye mkataba wa 2017 CBA na kutoa shilingi bilioni 2.4 kufanikisha ajira kwa madaktari wanafunzi 3,700. aidha amesema kuwa pesa hizo zitarejeshwa kwa hazina ya kitaifa iwapo KMPDU itakataa hatua hiyo ya serikali.Muriuki amewataka madaktari kurejea kazini mazungumzo yakiendelea.