Jude Mbaku ni mwanahabari mwingine, na mhariri mkuu wa DMRTV Buea,
mkaguzi mkuu wa kuhakiki habari za kweli katika eneo ambalo hapo awali
liliathiriwa na habari potofu. Mbaku anasema ameona makundi yanayotumia
mitandao ya kijamii kupotosha umma, na matokeo yake ni makubwa.
Jude Mbaku wa DMRTV Buea -Mhariri Mkuu anasema: Timu ya Cameroon ilipokwenda Cote d’Ivoire kwenye michuano ya Kombe la
Mataifa ya Afrika, tetesi zilienea kwamba Njie Clinton amejiuzulu kwenye
kikosi. Na walioeneza habari hizi walikuwa wapiganaji waliojitenga. Hili
halikufanywa kama jambo la makosa. Ilikuwa imeandaliwa vizuri na
kutayarishwa vyema ili kupotosha watu.
Karloff anasema kuwa waandishi wa habari wa Cameroon wanakabiliwa na
changamoto nyingi katika kuripoti kwa usahihi, ikiwa ni pamoja na ufadhili
mdogo, hatari za usalama, na upatikanaji mdogo wa habari.
Boris-Kaloff Meneja wa kituo cha CBS Buea anatoa maelezo zaidi:
"Nchini Cameroon, ni vigumu kupata takwimu na data. Unajua, nimekwenda
kwa wajumbe wa kanda wa usafiri kuulizia takwimu za magari yaliyosajiliwa
kusini-magharibi, haswa huko Buea, na nikaambiwa niende kusimama
barabarani kuanza kuhesabu magari mimi mwenyewe."
Ripoti ya Njodzeka Danhatu wa VOA, Buea, Cameroon.
#timu #mpira #cameroon #voa #voaswahili #njieclinton #cotedivoire #judembaku #dmrtvbuea #mharirimkuu #voa #voaswahili #habaripotofu