Mhubiri wa kanisa la Good News International Paul Mackenzie afikishwa mahakamani

  • | Citizen TV
    5,461 views

    Mhubiri wa kanisa la Good News International Paul Mackenzie amefikishwa mahakamani ambapo anatuhumiwa kwa kuhusika na mauaji ya baadhi ya waumini wake. Mackenzie na washukiwa wengine wanane wamefikishwa katika mahakama ya Malindi baada ya upande wa serikali kuomba siku 14 kuendelea na uchunguzi. Muda huo sasa umekamilika na washukiwa wamefikishwa mahakamani kwa mwelekeo zaidi.