Mikakati ya viongozi ya kupata mgao zaidi wa keki ya taifa Mlima Kenya

  • | K24 Video
    135 views

    Shilingi moja, kura moja na jinsi ya kuboresha kilimo kwa wakulima wa eneo la mlima Kenya ni ajenda kuu za kikao cha jioni ya leo cha viongozi kutoka mlima kenya, kinachoendelea katika uwanja wa gofu wa Nyeri. Zaidi ya wakazi 2000 wa eneo la mlima wakiwemo viongozi, wafanyabiashara na wasomi wanahudhuria kikao hicho kilichoandaliwa na naibu rais Rigathi Gachagua.