Kaunti ya Migori ni moja ya kaunti ambazo mimba za mapema zimekuwa zikitatiza masomo ya mtoto wa kike. Kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la UNICEF kati ya wasichana 4 wenye umri kati ya 15 to 19 , mmoja ametungwa mimba.
Wadau katika sekta ya Elimu kaunti ya Migori wanaashiria changamoto za mimba za mapema kwa umasikini ambao umekita mizizi katika jamii, kutokuwa na ufahamu kamili, kukosa Elimu katika maswala ya afya na Mila potovu katika jamii. Wadau hao wamezindua Shule ya bweni Kwa wasichana wanaopitia changamoto katika jamii na kuwaleta pamoja kielimu na mafunzo kama njia ya kukomesha mimba za mapema katika jamii haswa wadi ya Muhuru.