Mipango ya kutupilia mbali vituo maalum vinavyotoa matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV.

  • | K24 Video
    11 views

    Wizara ya afya imetangaza mipango ya kutupilia mbali vituo maalum vinavyotoa matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya HIV. Mpango huu unalenga kupunguza unyanyapaa na kutoa huduma za afya kwa kina kwa kuunganisha huduma za hiv katika vituo vya afya vya kawaida. Zaidi ya wakenya milioni 1.3 wanaoishi na hiv watafaidika kutokana na mpango huu, na kuwawezesha kupata huduma mbalimbali za afya pamoja na wagonjwa wengine.