Skip to main content
Skip to main content

Mirriam Chepkemoi awaleta pamoja kina mama 180 Narok kupitia mradi wa ‘KICK FOR HEALTH’

  • | Citizen TV
    359 views
    Duration: 5:00
    Amekuwa tumaini la faraja hasa kwa akina mama waliostaafu na walio na miaka 50 na Zaidi. Mirriam Chepkemoi mkaazi wa Narok amekuwa akiwaleta pamoja kina mama takriban 180 kwa mazoezi ndani ya timu nne za soka chini ya mradi wa ‘KICK FOR HEALTH’. Kundi hilo hukutana kwa mazoezi, kushauriana kuhusu maisha na kujikuza kibiashara. Ni harakati ambazo nyengine alizianza kitambo tangu alipokuwa mwanamke wa kwanza Diwani mwaka wa 1997 katika kata ya Loita mkoa wa Narok. Hebu tusikize simulizi yake kwa kina katika Makala yetu ya mwanamke bomba yanayofuata sasa