Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali asema Kenya Power inakabiliwa na madeni mengi

  • | Citizen TV
    1,796 views

    Hayo yakijiri, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali sasa ametoa taarifa kuhusiana na usimamizi wa kampuni ya umeme ya Kenya power kuhusu namna usimamizi wa miradi kadha ulivyoathiri utoaji wa huduma bora kwa wateja wake. Kenya power katika taarifa yake kwenye ripoti hiyo imelaumu kesi za mara kwa mara na baadhi ya wanakandarasi wanaoathiri shughuli za Kenya power.