- 832 viewsTaharuki imetanda katika eneo la kivu kusini, mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, saa chache baada ya mkataba wa makubaliano kutiwa saini ili kurejesha amani katika DRC. Mkataba huo uliotiwa saini na rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa DRC Felix Tshisekedi unatarajiwa kuondoa silaha mikononi mwa wapiganaji wote wakiwemo wale wa M-23, na kuwafungulia mashtaka waliohusika kwenye mauaji ya mamilioni ya watu.