Mkewe wa naibu Rais Dorcas Rigathi anazindua kituo kipya cha urekebishaj kaunti ya Nyeri

  • | Citizen TV
    472 views

    Mke wa naibu Rais Dorcas Rigathi anatarajiwa kufungua rasmi kituo cha urekebishaji tabia kwa waraibu wa pombe na dawa za kulevya kupindukia katika eneo bunge la Tetu kaunti ya Nyeri. Kumekuwa na juhudi za serikali za kupambana na ulevi katika eneo la kati na uuzaji wa pombe haramu na dawa za kulevya na kituo hiki kinatarajiwa kuwasaidia waraibu wa pombe na mihadarati.