Mkutano wa mawaziri | Rais Ruto aongoza kikao cha pili

  • | KBC Video
    21 views

    Matayarisho ya mitihani ya kitaifa ya mwaka huu ya wanafunzi wa gredi ya sita, darasa la nane na kidato cha nne itakayoanza tarehe 28 mwezi Novemba hadi tarehe 23 mwezi Disemba yanaendelea kufanywa. Hii ilithibitishwa leo wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri wanaoondoka ulioongozwa na Rais William Ruto.Wakati wa mkutano huo wa pili na baraza la mawaziri la aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta, Rais pia aliarifiwa kuhusu marekebisho yanayoendelea ya utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote kupitia kwa utekelezaji wa sheria itakayo hakikisha waajiri wote wanatoa malipo ya kila mwezi ya wafanyakazi wao kwa hazina ya kitaifa ya bima ya hospitali.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #williamruto #News